728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 19, 2016

    Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO).



    Endeleeni kuhesabu, ndiyo lugha rahisi unayoweza kuitumia baada ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kuendelea kuzifumania nyavu za wapinzani katika Ligi Kuu nchini England, Premier League.
       
    Manchester United ilicheza na Southampton katika mchezo wa pili wa Ligi hiyo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

    Zlatan Ibrahimovic alifungua akaunti ya mabao katika mchezo huo baada ya kumalizia kazi nzuri ya Wayne Rooney na kuipatia United bao la kuongoza.

    Mpaka mapumziko bado United ilikuwa mbele, ziliporejea kutoka vyumbani, ilimchukua dakika nane tu kuipatia timu yake bao la pili na la ushindi kwa njia ya penalti.

    Mchezo huo ulitawaliwa na jina kubwa lililoteka hisia za wengi, Paul Pogba na baada ya kufunga bao la pili, Ibrahimovic alishangilia nae.

    Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ibrahimovic alisema kwamba wanauchukulia ushindi huo kama njia ya kupata ushindi mwingine kwa mchezo ujao.

    Tazama Video ya Magoli ya Mchezo husika hapa chini. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO). Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top