728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 5, 2016

    Sasa ni Liverpool na Sevilla Fainali May 18 mjini Basel Switzerland.



    Liverpool imetinga fainali ya Europa League baada ya kuifunga Villarreal ya Hispania 3-0 na hivyo kupenya kwa jumla ya 3-1, hiyo ikiwa ni baada ya kufungwa 1-0 ugenini Alhamisi iliyopita.

    Klabu hiyo ya England sasa itakutana na Wahispania wengine - Sevilla kwenye fainali itakayochezwa Mei 18 huko BasEL, Switzerland. Sevilla imeifunga 3 - 1 Shakhtar Donetsk na kuingia fainali kwa jumla ya mabao 5-3.

    Beki Bruno Soriano wa Villarreal ndiye aliyefungua kitabu cha magoli baada ya kujifunga dakika ya saba katika juhudi zake za kuokoa krosi ya Roberto Firmino.

    Klabu ya Liverpool Ikishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wake waliojazana Anfield, Liverpool ikafunga bao la pili  kupitia kwa Daniel Sturridge dakika ya 63 huku Adam Lallana akitupia wavuni goli la tatu dakika ya 81.

    Picha zaidi hapa chini....





     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Sasa ni Liverpool na Sevilla Fainali May 18 mjini Basel Switzerland. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top