728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 5, 2016

    Ukweli Kuhusu Mahrez kama ataondoka Leicester City msimu ujao?

    Wakala wa mchezaji Reyard Mahrez, Kamel Bengougam amesema mchezaji huyo anaweza akabaki kwenye timu ya Leicester City au akaondoka msimu ujao.

    Mpaka sasa mchezaji huyo amefanikiwa kufunga magoli 17 na kutoa pasi 10 za mwisho, lakini kubwa zaidi Mahrez amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Uingereza PFA.

    “Ndiyo bila shaka kuna uwezekano Mahrez akaondoka msimu ujao, ningependa kusema ni 50-50 kama aendelea kuwepo au ataondoka. Huu umekuwa ni msimu wa ajabu na kuvutia kwa Mahrez na anafuraha sana kucheza Leicester City,” alisema wakala huyo.

    Aliongezea pia, “ana furaha sana Leceister City itacheza ligi ya mabingwa mwakani lakini kama atakuwa na mawazo ya kuchezea timu kubwa tutalifikiria hilo.”

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ukweli Kuhusu Mahrez kama ataondoka Leicester City msimu ujao? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top