
The Gunners waliruhusu mabao mawili
‘ya usiku’ na kupoteza nafasi kibao nzuri za kufunga na sasa wana kazi ya
kupiku ushindi wa mabao 2-0 waliopata Barca katika mechi ya awali iliyopigwa
Emirates.
Wengi wanaamini kwamba tayari Arsenal imetupwa nje ya Champions
League, lakini beki huyo raia wa Ujerumani anataka kuona wachezaji wenzake
wakipambana kiukweli na akasisitiza kuwa watajaribu kushambulia mwanzo mwisho
hadi kieleweke.
“Hatuwezi kukiri kushindwa,”
aliliambia gazeti la Evening Standard. “Tunakwenda huko na kujaribu kushambulia
bila kujali. Huo ndio uwezekano pekee tulionao. Tunaweza kuwa na bahati kwa
mechi hiyo kubwa kuwa upande wetu, lakini siwezi kutabiri, ni ngumu
kwelikweli.”
0 comments:
Post a Comment