Kocha mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema hali ya hewa nzito
ilichangia kufungwa mabao 2-0 na wenyeji African Sports Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hapo
jana.
Hatukuwa na hali nzuri kimchezo, hali nzito ya hewa imetuathiri
sana, tumecheza kukiwa na kiwango kikubwa cha joto, hata hivyo ndivyo
matokeo ya soka yalivyo tulichokitarajia hakikuwa, tunakwenda Songea
kwa mchezo mwingine, imani yangu tunaweza kupata ushindi huko” alisema.
Katika mchezo wa jana, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika
kwa timu hizo zikiwa hazijafungana,licha ya kuwepo kwa mashambulizi
kadhaa pande zote mbili ikiwemo lile la dakika ya 15 lililofanywa na
Abdalah Juma wa City aliyefanikiwa kuwatoka mabeki wa Sports, lakini
shuti lake likashindwa kulenga lango.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Sports kwani walipanga
mashambulizi vizuri na kufanikiwa kulifikia lango la City mara kadhaa
ikiwemo dakika 60 ambapo Omary Ibrahim alifanikiwa kuiandikia timu
yake bao la kuongoza kwa mpira mzuri wa adhabu kufuati yeye mwenyewe
kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la City.
Mpira ukiwa unaelekea ukingoni Ibrahim tena alifanikiwa kufunga bao
la pili kwa Sports baada ya kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Salum
Isihaka na kufanikiwa kuwatoka walinzi wa City kisha kufunga akiwa
pembeni kidogo mwa lango.
0 comments:
Post a Comment