728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 15, 2016

    ALICHOKISEMA PER MERTESACKER KUELEKEA MCHEZO WAO NA FC BARCELONA TAYARI NIMEKUWEKEA HAPA:


    PER mertesacker amesema Arsenal inakwenda Nou Camp kwa kazi moja tu ya kufanya maajabu na kuwachapa Barcelona katika mechi ya marudiano ya Champions League hatua ya 16 bora itakayopigwa Jumatano usiku.


    The Gunners waliruhusu mabao mawili ‘ya usiku’ na kupoteza nafasi kibao nzuri za kufunga na sasa wana kazi ya kupiku ushindi wa mabao 2-0 waliopata Barca katika mechi ya awali iliyopigwa Emirates. 

    Wengi wanaamini kwamba tayari Arsenal imetupwa nje ya Champions League, lakini beki huyo raia wa Ujerumani anataka kuona wachezaji wenzake wakipambana kiukweli na akasisitiza kuwa watajaribu kushambulia mwanzo mwisho hadi kieleweke.



    “Hatuwezi kukiri kushindwa,” aliliambia gazeti la Evening Standard. “Tunakwenda huko na kujaribu kushambulia bila kujali. Huo ndio uwezekano pekee tulionao. Tunaweza kuwa na bahati kwa mechi hiyo kubwa kuwa upande wetu, lakini siwezi kutabiri, ni ngumu kwelikweli.”



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ALICHOKISEMA PER MERTESACKER KUELEKEA MCHEZO WAO NA FC BARCELONA TAYARI NIMEKUWEKEA HAPA: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top