728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 13, 2016

    Udaku unaosambaa kuwa Diamond amepima DNA na Mwanae ni kweli? majibu je?.


    Sometimes ‘Wambea’ huwa na data kamili, lakini hufikisha bila ruhusa, udaku  hua unasababisha mivurugano lakini kuna udaku mwingine huleta furaha na kuzidisha faraja kwa baadhi ya watu .

    Kinachoendea katika mitandao mbali mbali ya ‘udaku’ Afrika Mashariki ni eti Diamond ameamua kupima vinasaba vya damu (DNA) ili kubaini kwamba Latiffah ‘Tiffah’ ni damu yake ama laa.

    Kizizi cha taarifa hizi kinasema kipimo hicho kimafanyika Afrika Kusini siku chache kabla staa huyu hajaenda Las Vegas.
     Gazeti la Amani kutoka Tanzania pia limeripoti kufanya mahojiano na Diamond Platnumz.

    “Kutokana na maneno maneno ya watu, ilifika mahali alichoka, akawa njia panda. Hivyo ili kuondoa figisu figisu, akamwambia Zari waende wakampime DNA mtoto na yeye. Ni kabla hajaenda Marekani.” alisema Chibu.

    Vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa Tiffah Dangote ni mtoto wa Diamond na sio mtoto wa billionaire Ivan Ssemwanga ambaye ni Ex wa Zari aliyekaa naye kwa miaka 10.

    Kwa mtazamo wa Tamaduni za Kitanzania na ‘Ushababi’, nachelea kuliamini hili kwa dhati kwa kuwa Diamond ni miongoni mwa wasanii thabiti wasioyumbisha na ‘Kijini tope’ cha aina yoyote ile, lakini kama ni kweli good for him ‘kauridhisha mtima wake’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Udaku unaosambaa kuwa Diamond amepima DNA na Mwanae ni kweli? majibu je?. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top