728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 15, 2016

    MASTAA WATAKATIMULIWA KWENYE UJIO WA ANTONIO CONTE NDANI YA CHELSEA ORODHA YAO IMETOKA …



    Antoni Conte anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Chelsea wenye thamani ya pauni milioni 18 na kuthibitishwa kuchukua nafasi ya kocha wa mpito.

    Guus Hiddink wakati wowote kutoka sasa, na tayari anaelezwa kujiandaa kufyeka mastaa 10 wa timu hiyo na kuingia na watano wapya.



    Kwa mujibu wa Express Sport, wachezaji wanaotarajiwa kufunguliwa mlango wa kutoka Stamford Bridge ni Eden Hazard, Oscar, Willian, Nemanja Matic, Loic Remy, John Terry, Diego Costa, Radamel Falcao, Alexandre Pato na Pedro.



    Gazeti la The Times limedai kuwa Conte atawasilisa kwa bilionea Roman Abramovich kumpatia fungu la kutosha kuweza kusajili mastaa watano wapya kiangazi hiki.



    Radja Nainggolan na Miralem Pjanic wa Roma, mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani na beki wa Juventus, Leonardo Bonucci ni miongoni mwa mastaa wanaopigiwa hesabu na Conte.



    Tayari pia Conte ameripotiwa kuanza mchakato wa kuhakikisha anakwenda Stamford Bridge pamoja na Mkurugenzi wa Michezo wa AS Roma ya Italia, Walter Sabatini.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MASTAA WATAKATIMULIWA KWENYE UJIO WA ANTONIO CONTE NDANI YA CHELSEA ORODHA YAO IMETOKA … Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top