728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 12, 2016

    Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje?

    Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na  Uzima, Josephat Gwajima, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), baada ya kushuka katika ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) akitokea  nchini Kenya.

    Askofu Gwajima, alikamatwa jana asubuhi na makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamepiga kambi eneo hilo, baada ya kupata taarifa za kuwasili kwake.

    Vyanzo vya habari kutoka kwa watu wa karibu na Askofu Gwajima, vilisema  kuwa baada ya kiongozi huyo wa kiroho kushuka katika ndege, alitakiwa kupanda helikopta yake ili aelekee Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Masaki, Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko.

    Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Sea Cliff, Askofu Gwajima, alijikuta akiishia mikononi mwa polisi na kupelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa

    Vyanzo hivyo vilidai kuwa baada ya kufikishwa kituoni, alipelekwa kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na baadaye  ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo, Camillus Wambura.

    “Askofu Gwajima alikamatwa uwanja wa ndege na polisi akitokea nje ya nchi na kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu na kuhojiwa, lakini ameachiwa kwa dhamana na simu zake za  kiganjani zinashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi,” kilisema chanzo hicho.

    Msemaji wa kiongozi huyo wa kiroho, Yekonia Behagaze, alikiri kiongozi wao kukamatwa.

    “Ni kweli Askofu Gwajima amekamatwa na polisi leo (jana) asubuhi akitokea nje ya nchi, alihojiwa kwa saa nne,” alisema.
    Alisema baada ya kumaliza mahojiano hayo, aliachiwa kwa dhamana ili aendelee  na majukumu yake.

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Sirro,  alithibitisha kukamatwa kwa Askofu Gwajima.
    “Ameletwa, amehojiwa, amepewa dhamana na uchunguzi unaendelea,” alisema.

    Chanzo: Mtanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top