728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, September 17, 2015

    Auawa akizuia mifugo isile mahindi shambani mwake




    Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia wananchi wawili jamii ya wafugaji,kwa tuhuma za kumpiga hadi kumsababishia kifo mkazi wa Tindiga,tarafa ya Masanze wilayani kilosa,baada ya kujaribu kuwazuia wasilishie mifugo katika shamba lake la mahindi ambapo wananchi wenye hasira kali wamelipiza kwa kuwaua ng'ombe 68 kutokana na mauaji hayo.

    Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema mauaji ya mtu huyo,Said Sandali (42) mkazi wa Tindiga Kilosa, yametokea baada ya kujaribu kuwazuia wafugaji wasilishe mifugo kwenye shamba lake la mahindi,lakini wafugaji hao walimpiga hadi kusababisha kifo chake,jambo lililowatia hasira wana jamii wa eneo husika,ambao wamevamia ng’ombe 108 na kuwakata kata kwa mapanga, na kati yake 68 wakapoteza maisha.

    Kufuatia tukio hilo kamanda huyo wa polisi ametoa wito kwa makundi ya wakulima na wafugaji  kuheshimiana na kuacha kujichukulia sheria mikononi, na  kuzishauri serikali za vijiji kushirikiana na watu wanaoheshimika na makundi yote kuunda sheria ndogo ndogo watakazozisimamia na kuzitekeleza,ambapo wananchi wametaka elimu ya uraia kuzidi kutolewa ili jamii ijitambue na wanasiasa kuacha kuwa chanzo cha uchochezi ili kuondoa matatizo kama hayo yanayojitokeza.

    Tukio jingine limehusisha kukamatwa kwa vijana wawili kwa tuhuma za kufanya vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani,kwa kutembea usiku wakiwa wamebeba mfano wa majeneza yenye vitambaa vya kijani.
     edwinmoshi.blogspot.com

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Auawa akizuia mifugo isile mahindi shambani mwake Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top