728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 2, 2016

    MAJIBU YA EL CHAPO KUTOROKA JELA YAKO HAPA.

    Habari  zinaenea kwenye mitandao ya kijamii na hasa Twitter kwamba mlanguzi hatari wa dawa za kulevya Joaquin Guzman, maarufu kama EL Chapo ametoroka jela tena.
    Je, zilikuwa za kweli?


    La hasha. Habari hizi zilitokana na tovuti ya habari za kubuni ya abcnews.com.co ambayo imefanywa kuonekana kana kwamba ni ya shirika tajika la habari la Marekani la ABC News ambalo tovuti yake halisi ni abcnews.go.com.

    Habari hizo za kubuni, zilieleza jinsi walinzi wawili wa gereza walivyoonekana wakiwa wamemshika El Chapo, kana kwamba wanamhamisha kutoka seli moja hadi nyingine, mwendo wa saa nane usiku na baadaye ikadaiwa kwamba ametoweka pamoja na walinzi hao.
    Muda mfupi baadaye, habari hizo zinasema gari la gereza lilipatikana likiwa limeachwa umbali wa maili moja hivi kutoka gerezani.
    Wengi waliamini habari hizo na wakaanza kujadili kutoroka kwake jela kana kwamba ni tukio lililokuwa limefanyika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAJIBU YA EL CHAPO KUTOROKA JELA YAKO HAPA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top