Label ya The industry inayo ongozwa na Navy Kenzo (Nahreel na Aika)
wameongeza wasanii wapya kwenye Label hiyo na kuwatambulisha leo hii.
Rosaree huyu ni mwanadada ambaye anakipaji cha kurap ambaye anajiita
Rap Goddess akiwahadi mashabiki wa muziki nchini wawe tayari kusikia
ukali wake kwenye gemu ya kurap.
Msanii mwingine kujiunga na label hiyo ni Selene huyu ni mwanadada
ambaye anaimba,naye amepata fursa ya kuweza kujiunga na kundi hili la
the Industry.
Label hii pia hakuangalia tu wanadada warembo bali pia waliweza
kumchagua Kijana anayenda kwa jina la willdad ambeye yeye anakipaji cha
kucheza na kuimba kwa pamoja.
Kiongozi wa Label hiyo Nahreel alielezea jinsi gani watakuwa
wakifanya kazi kwa pamoja na kuonyesha vipaji vya wasanii wapya kwenye
label hiyo mpya.
kwa maelezo zaidi sikiliza show nzima ndani ya the Playlist na
Chipuka wikendi hii upate kujia uanzilishi na nini cha kutarajia kutoka
kwa wasanii hao wapya wa kwenye label hiyo.
![]() |
Msanii mpya mwingine mpya wa The Industry Rosaree |
![]() |
Selena Msanii mwingine mpya kutoka The Industry |
![]() |
0 comments:
Post a Comment