Jeshi la polisi mkoani
Morogoro linawashikilia wananchi wawili jamii ya wafugaji,kwa tuhuma za kumpiga
hadi kumsababishia kifo mkazi wa Tindiga,tarafa ya Masanze wilayani
kilosa,baada ya kujaribu kuwazuia wasilishie mifugo katika shamba lake la
mahindi ambapo wananchi wenye hasira kali wamelipiza kwa kuwaua ng'ombe 68
kutokana na mauaji hayo.
Kamanda wa Polisi mkoa
wa Morogoro Leonard Paulo amesema mauaji ya mtu huyo,Said Sandali (42) mkazi wa
Tindiga Kilosa, yametokea baada ya kujaribu kuwazuia wafugaji wasilishe mifugo
kwenye shamba lake la mahindi,lakini wafugaji hao walimpiga hadi kusababisha
kifo chake,jambo lililowatia hasira wana jamii wa eneo husika,ambao wamevamia
ng’ombe 108 na kuwakata kata kwa mapanga, na kati yake 68 wakapoteza maisha.
Kufuatia tukio hilo
kamanda huyo wa polisi ametoa wito kwa makundi ya wakulima na wafugaji
kuheshimiana na kuacha kujichukulia sheria mikononi, na kuzishauri
serikali za vijiji kushirikiana na watu wanaoheshimika na makundi yote kuunda
sheria ndogo ndogo watakazozisimamia na kuzitekeleza,ambapo wananchi wametaka
elimu ya uraia kuzidi kutolewa ili jamii ijitambue na wanasiasa kuacha kuwa
chanzo cha uchochezi ili kuondoa matatizo kama hayo yanayojitokeza.
Tukio jingine
limehusisha kukamatwa kwa vijana wawili kwa tuhuma za kufanya vurugu na
kusababisha uvunjifu wa amani,kwa kutembea usiku wakiwa wamebeba mfano wa
majeneza yenye vitambaa vya kijani.
edwinmoshi.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment