Mbio za Mwenge wa Uhuru zimetua
Kanda ya ziwa huku zikizua sintofahamu kwa watumishi wa umma waliotakiwa
kutokukosa mkesha wake ili kukwepa rungu la Mamlaka za kinidhamu dhidi yao.
Taarifa kutoka wilayani Sengerema
zilieleza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ameagiza watumishi wote
wa wilaya hiyo kuhakikisha wanahudhuria mkesha huo na kwamba daftari la
mahudhurio litaitishwa majira ya saa 6 usiku, saa 9 usiku na saa 12 usiku.
Hayo yamebainishwa katika Tangazo
rasmi lililosainiwa na Msangi M.A kwa niaba ya Mkurugenzi, Magessa Boniface.
Aidha, katika Wilaya ya Nyamagana
mkoani Mwanza, imeelezwa kuwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari
waliitwa katika kikao na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mary Tesha ambaye aliwaeleza kuwa
ambaye hatahudhuria mkesha huo atakumbwa na adhabu ikiwa ni pamoja na kushushwa
vyeo.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya
alipotafutwa, alikana kuwaeleza walimu hao kuwa wangeshushwa vyeo kama
wasingehudhuria ingawa alikiri kuwa alikutana nao.
“Sijasema hayo, nilichosema ni kuwa
Mwenge ni jukumu letu watumishi tunapaswa kushiriki. Hao walimu ni wajumbe wa
Kamati za Mbio za Mwenge hivyo wanapaswa kushiriki. Hilo la kufukuza,
kuwawajibisha hapana,” alisema Tesha.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) wilaya ya Nyamagana, Asha Juma alisema kuwa ingawa amesikia kuwepo kwa
maagizo hayo, hajapata malalamiko kutoka kwa walimu.
“Najuwa wanahamasisha watumishi
waende, lakini nadhani wangetafuta njia nyingine ya kuwahamasisha sio vitisho,”
alisema Katibu huyo wa CWT.
Duuuuuh. kama ndo hivo shida ndo kitu ambachooo. watu sometime tunaishi kwa nidham ya uwoga sana na tutajikuta tu tunafeli kusonga
ReplyDelete