Makamu Mwenyekiti
wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani
Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi hii leo Jijini
Mwanza kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki
yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja
vya Rock City Jijini Mwanza.
Wengine ni, Hassan
Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto),
Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani
Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia), kutoka bodi
ya Washauri TCCIA.
Makampuni pamoja na wajasiriamali
mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, yametakiwa
kutumia Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki katika kutangaza na
kuuza bidhaa zao.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya
Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard
Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo.
"Maonesho haya yanatoa fursa kwa
makampuni mbalimbali Afrika Mashariki kujitangaza, kukutana na wateja
wao, kutafuta wabia wapya wa kibiashara pamoja na kufanya utafiti wa
kimasoko". Ametanabaisha Lema.
Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza
agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall
Jijini Mwanza na yanatarajiwa kushirikisha wafanyabiashara kutoka
mataifa ya Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki.
Picha zaidi
Picha zaidi hapa chini.
Picha na BMG.
0 comments:
Post a Comment