Baada ya kutangaza kuvunja mkataba wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda,
Haruna Niyonzima, Katibu wa klabu hiyo Dr Jonas Tiboroha sasa amekalia
kuti kavu kutokana na kudaiwa kufanya maamuzi ya kukurupuka.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo yenye makao yake mitaa ya Twiga na
Jangwani zimesema, uongozi huo tayari unapanga kuachana na Tiboroha
ifikapo Januari Mosi 2016.
Hivi karibuni Tiboroha aliwagawa wanachama wa klabu ya Yanga,
kufuatia kuvunja mkataba na Niyonzima, huku pia akimtaka mchezaji huyo
kuilipa klabu hiyo dola za kimarekani 71,000 sawa na milioni 149 za
fedha za kitanzania.
Sababu zilizotolewa kupelekea kuvunja mkataba huo ni kushiriki
michuano isiyotambulika ya CECAFA, jambo ambalo wadau wa soka
limewashangaza kwani michuano hiyo inatambulika na CAF, FIFA na Tanzania
akiwa mwanachama wa michuano hiyo, iliyopelekea kusimamishwa kwa Ligi
Kuu ya Vodacom kutoa nafasi kwa Kilimanjaro kushiriki michuano hiyo.
Kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda AMAVUBI bila mwaliko, taarifa
zinaonyesha Haruna Niyonzima ana barua za mwaliko kwa kila kalenda ya
FIFA kutoka shirikisho la mpira la nchini Rwanda, FERWAFA kumuomba
mchezaji huyo kuitumikia timu yake ya Taifa na barua hiyo kutumwa TFF na
nakala kwenda klabu ya Yanga.
Kuchelewa kurudi anapokua Rwanda, mchezaji Niyonzima amewahi kupewa
onyo kwa mdomo mara moja tu bila maandishi yoyote, kitu ambacho kisheria
hakina ushahidi.
Kufuatia sababu hizo zilizotolewa na Yanga kupelekea kuvunja mkataba
dhidi ya Niyonzima, zimeonyesha hazina mashiko kwani katika mkataba wake
hakuna kipengele kinachoelezea juu ya kuvunja mkataba endapo mchezaji
atachelewa kurudi/kuripoti kwenye kituo chake cha kazi.
Mpaka sasa Yanga haijamkabidhi Niyonzima barua ya kuachana nae ikiwa
ni siku ya tatu tangu kutangaza kuachana nae kwa kukiuka mkataba.
Baada ya kupitia vifungu vya CAF na FIFA juu ya uvunjwaji wake
mkataba huo, uongozi wa Yanga umeona Katibu mkuu huyo amekurupuka bila
kujua sheria zinazoongoza soka duniani zinaelekeza nini, na kuifanya
klabu hiyo sasa kuwaza njia ya kumlipa mnyarwanda huyo pesa zake kwa
kuvunja mkataba.
Pamoja sana mpapuki
ReplyDelete