![]() |
Maiti ya mvulana wa Kisyria, Aylan Kurdi, ikiwa imelala ufukweni nchini Uturuki. |
Sunday, September 13, 2015
Licha ya picha ya maiti ya mtoto Aylan Kurdi wa Syria aliyekufa maji
akijaribu kuvuuka bahari kuingia Ulaya kuutikisa ulimwengu wa Magharibi,
mhariri mkuu wa DW, Alexander Kudascheff, anatetea kuchapishwa kwa
picha hiyo.
Picha hii kwa vyovyote inaonesha taswira ya kuhuzunisha. Inatuonesha
kitisho kinachowakabili watu wanaojaribu kuikimbia nchi
iliyokwishasambaratishwa kwa vita, Syria. Picha hii ni kielelezo cha
yale yanayotokea kila siku kwenye Bahari ya Mediterrenia.
Juu ya hayo, picha hii inaakisi pia ubaya wa vita hivyo vya wenyewe kwa
wenyewe. Ni taswira inayochafua nafsi. Ni picha inayomchoma mtu ndani
kabisa ya hisia zake kwa mshindo. Inakusuta ikikwambia kuwa wewe huna
maana. Inakufanya ufikirie mara mbili mbili, lakini bado ni picha
inayotunyamazisha sote.
Hii ni picha ambayo sote tunaihisi - ni picha ya mwaka, na yumkini hata
ya muongo mzima. Inasimamia kila kile ambacho kinatushitua, kinatugusa,
kinatukasirisha na kutupandisha ghadhabu kwa miezi kadhaa sasa. Na ni
picha ya kuhuzunisha.
Lakini swali kubwa kwenye tasnia yetu ya habari ni ikiwa kweli
tunaweza au tunapaswa kuionesha? Kuna sababu zinazoshawishi kwamba
tusifanye hivyo. Sababu za heshima kwa utu wa kitoto hiki na mahitaji
yenye uhalali kutoka kwetu watu wa vyombo vya habari.
Tunaichapisha kwa uzito wake
Ila kwa makusudi kabisa, tumeamua kuionesha. Sio kwa kuzusha hamasa, sio
kwa kusaka "clicks" nyingi zaidi kwenye kurasa zetu, sio kuwania
dhamira yetu ya kuelekea kwenye matangazo ya televisheni. Hapana.
Tunaionesha kwa kuwa inatugusa sote. Tunaionesha kwa kuwa ni alama ya
balaa la mzozo wa sasa wa wakimbizi.
Masikini, wazazi wasio hatia wa kitoto walilazimika kukichukuwa kwenda
nacho safari ya hatari kusaka mustakabali mwema, safari yao ikaishia
kwenye mauti ya baharini, nacho kikasombwa ufukweni kuja kutusimulia
sisi tulio hai hadithi yake.
Kwa hivyo, tunaionesha picha hii kwa sababu imetutikisha na kwa sababu
kwenye mkutano wa jopo la wahariri tulijikuta tumesinzima na kuduwazwa.
Tumeguswa na mateso na mauti. Tunaionesha kwa kuwa tumeumizwa sana na
mateso haya, na kwamba licha ya pirika na harakati zote kwenye kazi zetu
kama waandishi wa habari, tumejikuta tumepoozeshwa na picha hii.
Mwandishi: Alexander Kudascheff
Related Posts
Donny Roberty Mshindi Miss Mwanza 2016 Tazama Picha hapa chini.
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,20...
MAONESHO YA BIASHARA ROCK CITY MALL MWANZA.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda n...
TFF Yatoa Angalizo Kwenye Msimu Mpya Wa VPL 16-17.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17 inatarajiwa kuan...
Sumatra Imesema hakuna usafiri utakaositishwa.
MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewatoa hofu ...
Hesabu inaendelea Ibra aweka mbili Nyumbani (VIDEO).
Endeleeni kuhesabu, ndiyo lugha rahisi unayoweza kuitumia baada...
Mambo 8 Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
Kila wakati wengi wetu katika maisha, ni watu wa kujiwekea malengo....
Mkurugenzi Atishia Kuitisha Daftari la Mahudhurio saa tisa Usiku sababu Je?
Normal 0 false false false EN-U...
Gwajima atiwa Nguvuni na Polisi Dar, Imekuaje?
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata ...
Baada ya Cameroon huyu ndio kuwa Waziri mkuu wa Uingereza.
Katika saa au siku kadhaa zijazo, Waziri wa maswala ya nda...
ULIPITWA; MATOKEO YA ENGLAND VS RUSSIA YAKO HAPA.
June 11 2016 michuano ya Euro 2016 inayofanyika Ufaransa imeen...
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment