Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba
25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na
aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
Christopher Ryoba Kangoye.
Katika kesi hiyo,
wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche
(Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo
ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.
Baada ya Mahakama
hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua
kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja
za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya
waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.
Wakili wa mleta
maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja
aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Nae
Mwl.Chacha
Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara, ameelezea kuwa na imani na
Mahakama kutokana na maamuzi iliyoyatoa katika kesi hiyo pamoja na kesi
nyingine zilizowahi kuamuliwa Mahakamani hapo na kuongeza kuwa sasa kazi
imebaki moja kwa Mhe.Heche ambayo ni kuwatumikia wakazi wa Jimbo la
Tarime Vijijini.
Kwa upande wake Mrimi
Zabloni ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, ameelezea furaha
kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwasihi kuweka imani na Mahakama hapa nchini
katika kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.
Wananchi
wengi
Mahakamani hapo kutoka Jimboni Tarime Vijijini walikuwa ni wafuasi wa
Chadema
na wameonyesha kuyapokea maamuzi ya mahakama hiyo kwa furaha kubwa na
kwamba wao waliamua ushindi wa Heche tangu Novemba 25 mwaka jana kwenye
daftari la kupigia kura.
Kesi hiyo
ilisikilizwa January 19,2016 mwaka huu na kuahirishwa hadi juzi January 27,2015 kwa ajili
ya kutolewa maamuzi, lakini pia iliahirishwa hadi jana January 28,2016 ambapo maamuzi
yameweza kutolewa.
C
CHANZO BINAGIMEDIAGROUP.BLOGSPOT.COM
0 comments:
Post a Comment