728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 29, 2016

    Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa

    Kila kitu kilichopo dunia kinaongozwa na sheria zake. Sheria hizo zinapotumika ipasavyo mara nyingi sana huleta mafanikio makubwa. Na inapotokea sheria hizo zikavunjwa hakuna mafanikio yanayokuwepo zaidi ya kushindwa kwa wale wote waliovunja sheria hizo.


    Haijalishi upo katika eneo gani sheria ni muhimu sana kuzingitiwa. Iwe katika afya, elimu, mchezo wa mpira wa miguu, au biashara sheria huwa zipo na zinafanya kazi. Sheria hizi ndizo zinazotupa mwongozo bila kujali uwe unazijua au huzijui lakini zipo, ukikosea unahukumiwa.

    Katika makala hii tutajifunza sheria zitakazo kusaidia kufanya biashara yako kwa ushindi. Bila shaka umekuwa ukiona wengi wakifanya biashara zao kwa mazoea sana. Kutokana na mazoea hayo hupelekea biashara nyingi kugeuka kuwa kama ‘miradi bubu’ ambayo haina faida yoyote.

    Sitaki hilo lizidi kukutokea sana la kufanya biashara ambayo haikupi faida kubwa unayoifikiri kwa muda mrefu. Inabidi ukubali umekosea na kaa chini ujifunze sheria za msingi kabisa ambazo zinaweza kukusaidia kukutoa hapo na kukupeleka katika hatua nyingine ya mafanikio kibiashara.

    Zifuatazo Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa. 1. Toa huduma bora kwa wateja wako.
    Toa huduma bora itakayowafanya wateja wako waweze kujisikia vizuri na kushawishika kuja kununua tena kwa wakati mwingine. Kwa kutoa huduma bora itakusaidia sana kutokuendesha biashara yako kimazoea. Ila ikiwa utajisahau au kusahau sheria hii basi elewa utajitengenezea mazingira ya kushindwa kiurahisi kwenye biashara unayoifanya.

    2. Jijengee mazoea ya kuwa na lugha ya ukarimu.
    Hili ni jambo litakalokusaidia sana kukuza biashara yako kwa sehemu kubwa. Kuna wakati unakutana na wateja ambao ni wakorofi hawaeleweki. Tambua hutakiwi kuwaonyesha chuki wala kuwasemesha kwa lugha ya ukali. Toa lugha ya ukarimu wakati wote unapokuwa kwenye biashara yako.

    3. Jali sana muda wa wateja wako.
    Kitu kizuri kabisa kitakachokufanya uweze kujijengea uaminifu na kukuza wateja wako ni uwezo wako wa kujaali muda wa wateja. Muda ni kitu cha muhimu sana kwa mteja wako. Kwa namna yoyote ile usimpotezee mteja wako muda wake. Jitahidi sana kumhudumia katika muda mwafaka ambao amefika na sio kumchelewesha bila sababu ya msingi.

    4. Mazingira yako yawe safi.
    Kila wakati na kila siku, hakikisha mazingira ya unapofanyia biashara yako yawe safi. Lakini si mazingira tu hayo yawe safi bali hata wewe na wahudumu wako lazima muwe wasafi ili kuhakikisha kumvutia wateja katika eneo watakalo kaa. Hii ni sheria nzuri sana ambayo inaweza kupelekea kukuza wateja wako siku hadi siku.

    5. Weka matangazo ya biashara yako.
    Ni vyema ukajitengenezea matangazo ya biashara yako. Hakuna biashara ambayo inaweza ikakua sana bila kuwa na matangazo. Matangazo ni muhimu sana kwa biashara yoyote. Matangazo yanaisadia biashara yako kuweza kujulikana katika maeneo mengi ambayo ilikuwa sio rahisi kuweza kujulikana na kwa muda mrefu.

    Unapokuwa kwenye biashara muda wako wote hakikisha unafanya kile unachokisema. Simamia kauli zako, bila kuyumbishwa. Kama uliwaambia wateja wako mzigo utaletwa wiki ijayo , hakikisha hilo linatekelezeka pia. Kwa kifupi hapa hutakiwi kuwa mwongo. Toa taarifa sahihi zitakusaidia kukuza wateja wako na kuwa wengi.

    7. Kuwa mwangalifu na mtaji wako.
    Pamoja na kwamba biashara yako inaweza ikawa imeanza kukupa ile faida inayotarajiwa, lakini ili kuikuza na kuifanya kwa ushindi zaidi ni vyema ukawa mwangalifu na mtaji wako. Acha kutumia pesa zako hovyo sana ambazo zipo kwenye biashara. Tunza mtaji wako ukusaidie kuweza kuwekeza pia katika maeneo mengine muhimu.

    8. Jenga mazoea ya kujifunza siku zote.
    Hapa nikiwa na maana jifunze kutoka kwa wenzako wanafanya nini? Jifunze kwako pia hasa kile kipindi unapotokea umekosea. Ukikosea acha kujibebesha hasira ambazo zinaweza kukubomoa na kukuharibu. Badala yake kaa chini, kisha jifunze kwa nini umekosea katika hili. Na baada ya hapo rekebisha na endelea na safari.

    Kwa kuzijua sheria hizi zitakusaidia sana kuweza kuendesha biashara yako kwa ushindi na mafanikio makubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top