WAKALA wa mchezaji mahiri wa timu ya soka ya Manchenster United ya nchini Uingereza, Wayne Rooney, amesema kwamba mchezaji huyo hana mpango wa kutaka kutua nchini China kama inavyoripotiwa.
Taarifa iliyotolewa na wakala huyo, imeeleza kwamba mchezaji huyo hajawahi kukutana
na viongozi wa timu yoyote ya nchini humo na kueleza kwamba bado ana mkataba wa
kuitumikia Manchester United. Aliema yeye kama msimamizi wa mchezaji huyo, hana
taarifa yoyote ya mkali huyo kutakiwa nchini China kama inavyoripotiwa katika
baadhi ya vyombo vya habari.
Majuzi iliripotiwa kuwa klabu ya Shanghai SIPG
inayonolewa na kocha za zamani wa England Sven Goran Eriksson imetenga zaidi ya pauni
milioni 75 ili kumnasa Rooney. Katika taarifa hiyo inadaiwa kuwa klabu hiyo ipo
tayari kumpa Rooney mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya pauni milioni 25
kwa msimu.
0 comments:
Post a Comment