KOCHA aliye hatarini kupoteza
kibarua chake, Jose Mourinho amesema kwamba bado anaamini timu yake ya Chelsea
inaweza kuzinduka na kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya nne bora.
Hadi sasa, Chelsea
wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 15,
huku wakiwa wameshinda mechi moja kati ya sita za mwisho.
Nafasi ya vijana hao
wa Mourinho kufuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao ipo
mashakani kutokana na kwamba wako nyuma kwa pointi 14 dhidi ya timu inayoshika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi, Manchester United.
Hata hivyo, pamoja na
kuwa katika hali hiyo, kocha huyo raia wa Ureno ameshindwa kukata tamaa akisema
kwamba bado ana uwezo wa kutinga hatua hiyo ya nne bora. “Sio jambo rahisi kwa
klabu kubwa kushinda tatu ama nne mfululizo,” alisema kocha huyo.
“Kwasababu
hakuna ambaye ameshafanya hivyo, tuna nafasi ya kushinda na ndoto zetu ni
kumaliza tukiwa miongoni mwa timu nne bora na kimahesabu inawezekana,
tutajaribu kufanya hivyo.”
Mbali na kujipa matumaini hayo, kocha uyo mwenye
umri wa miaka 52 aliwapongeza mashabiki wa Chelsea ambao wameamua kuwa nae muda
wote kwa kipindi hiki kigumu kwake.
KOCHA aliye hatarini
kupoteza kibarua chake, Jose Mourinho amesema kwamba bado anaamini timu
yake ya Chelsea inaweza kuzinduka na kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya nne
bora.
Hadi sasa, Chelsea wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu
baada ya kucheza mechi 15, huku wakiwa wameshinda mechi moja kati ya
sita za mwisho.
Nafasi ya vijana hao wa Mourinho kufuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa
Ulaya msimu ujao ipo mashakani kutokana na kwamba wako nyuma kwa pointi
14 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi,
Manchester United.
Hata hivyo, pamoja na kuwa katika hali hiyo, kocha huyo raia wa Ureno
ameshindwa kukata tamaa akisema kwamba bado ana uwezo wa kutinga hatua
hiyo ya nne bora.
“Sio jambo rahisi kwa klabu kubwa kushinda tatu ama nne mfululizo,”
alisema kocha huyo. “Kwasababu hakuna ambaye ameshafanya hivyo, tuna
nafasi ya kushinda na ndoto zetu ni kumaliza tukiwa miongoni mwa timu
nne bora na kimahesabu inawezekana, tutajaribu kufanya hivyo.”
Mbali na kujipa matumaini hayo, kocha uyo mwenye umri wa miaka 52
aliwapongeza mashabiki wa Chelsea ambao wameamua kuwa nae muda wote kwa
kipindi hiki kigumu kwake.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/licha-ya-kukalia-kuti-kavu-jose.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/licha-ya-kukalia-kuti-kavu-jose.html
Copyright © saluti5
0 comments:
Post a Comment