728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, January 25, 2016

    MBUNGE WA NZEGA BASHE AMEYASEMA HAYA YAMFIKIE MEMBE BAADA YA KUMKOSOA RAIS MAGUFULI.


    Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe amemtaka aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kumshambulia Rais John Magufuli katika utendaji wake.
    Kauli ya Bashe imekuja siku moja baada ya mfululizo wa habari zilizomnukuu Membe akimkosoa Rais Magufuli katika maeneo kadhaa likiwamo suala la kuzuia safari za nje, Rais kwenda nje ya nchi huku akimpa tahadhari ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa.
    Kupitia taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, Bashe alisema Membe amekuwa waziri kwa miaka kumi na kutimiza wajibu wake, hivyo amuache Magufuli naye atimize wajibu wake kwa wananchi.
    “Aliomba urais, hajateuliwa, asubiri 2020 au 2025 ili akipita aanzishe ‘uvasko da Gama’ tena,” alisema
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBUNGE WA NZEGA BASHE AMEYASEMA HAYA YAMFIKIE MEMBE BAADA YA KUMKOSOA RAIS MAGUFULI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top