728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 1, 2016

    Niyonzima kuondoka na kichwa cha katibu mkuu Yanga.

    Baada ya kutangaza kuvunja mkataba wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima, Katibu wa klabu hiyo Dr Jonas Tiboroha sasa amekalia kuti kavu kutokana na kudaiwa kufanya maamuzi ya kukurupuka.


    Taarifa za ndani ya klabu hiyo yenye makao yake mitaa ya Twiga na Jangwani zimesema, uongozi huo tayari unapanga kuachana na Tiboroha ifikapo Januari Mosi 2016.
    Hivi karibuni Tiboroha aliwagawa wanachama wa klabu ya Yanga, kufuatia kuvunja mkataba na Niyonzima, huku pia akimtaka mchezaji huyo kuilipa klabu hiyo dola za kimarekani 71,000 sawa na milioni 149 za fedha za kitanzania.
    Sababu zilizotolewa kupelekea kuvunja mkataba huo ni kushiriki michuano isiyotambulika ya CECAFA, jambo ambalo wadau wa soka limewashangaza kwani michuano hiyo inatambulika na CAF, FIFA na Tanzania akiwa mwanachama wa michuano hiyo, iliyopelekea kusimamishwa kwa Ligi Kuu ya Vodacom kutoa nafasi kwa Kilimanjaro kushiriki michuano hiyo.
    Kujiunga na timu ya Taifa ya Rwanda AMAVUBI bila mwaliko, taarifa zinaonyesha Haruna Niyonzima ana barua za mwaliko kwa kila kalenda ya FIFA kutoka shirikisho la mpira la nchini Rwanda, FERWAFA kumuomba mchezaji huyo kuitumikia timu yake ya Taifa na barua hiyo kutumwa TFF na nakala kwenda klabu ya Yanga.
    Kuchelewa kurudi anapokua Rwanda, mchezaji Niyonzima amewahi kupewa onyo kwa mdomo mara moja tu bila maandishi yoyote, kitu ambacho kisheria hakina ushahidi.
    Kufuatia sababu hizo zilizotolewa na Yanga kupelekea kuvunja mkataba dhidi ya Niyonzima, zimeonyesha hazina mashiko kwani katika mkataba wake hakuna kipengele kinachoelezea juu ya kuvunja mkataba endapo mchezaji atachelewa kurudi/kuripoti kwenye kituo chake cha kazi.
    Mpaka sasa Yanga haijamkabidhi Niyonzima barua ya kuachana nae ikiwa ni siku ya tatu tangu kutangaza kuachana nae kwa kukiuka mkataba.
    Baada ya kupitia vifungu vya CAF na FIFA juu ya uvunjwaji wake mkataba huo, uongozi wa Yanga umeona Katibu mkuu huyo amekurupuka bila kujua sheria zinazoongoza soka duniani zinaelekeza nini, na kuifanya klabu hiyo sasa kuwaza njia ya kumlipa mnyarwanda huyo pesa zake kwa kuvunja mkataba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    Item Reviewed: Niyonzima kuondoka na kichwa cha katibu mkuu Yanga. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top