728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 29, 2016

    Maua Sama: Bila Mwana FA nisingekuwa hapa.

    STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama kwa mara ya kwanza amefungukia mafanikio yake kimuziki kwa kusema kuwa bila ya staa wa muziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ asingekuwa alipo saa.

    Akizungumza katika kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa na Global TV Online, Maua anayebamba na Ngoma ya Mahaba Niue alianza kwa kusimulia kwa jinsi alivyokutana na Mwana FA.

    “Ilikuwa kitu cha ajabu kwangu. Wimbo wangu wa kwanza kabisa kuuimba ulikuwa So Crazy na kipindi nimeuimba nilikuwa chuoni Moshi, basi marafiki zangu wakamtumia wimbo huo MwanaFA bila mimi kujua na baada ya wiki nikashangaa kupigiwa simu na Mwana FA akaniambia amependa ninavyoimba na kwamba yupo tayari kuni-meneji na pia kunishirikisha,” alisema Maua.

    Kwa picha zaidi cheki hapa chini..... 







    chanzo cha stori hii ni www.globalpublishers.co.tz
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Maua Sama: Bila Mwana FA nisingekuwa hapa. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top