728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 17, 2015

    LICHA YA KUKALIA KUTI KAVU, JOSE MOURINHO ANAAMINI CHELSEA ITATINGA TOP FOUR PREMIER LEAGUE

    KOCHA aliye hatarini kupoteza kibarua chake, Jose Mourinho amesema kwamba bado anaamini timu yake ya Chelsea inaweza kuzinduka na kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya nne bora.
    Hadi sasa, Chelsea wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 15, huku wakiwa wameshinda mechi moja kati ya sita za mwisho.

    Nafasi ya vijana hao wa Mourinho kufuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao ipo mashakani kutokana na kwamba wako nyuma kwa pointi 14 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi, Manchester United.

    Hata hivyo, pamoja na kuwa katika hali hiyo, kocha huyo raia wa Ureno ameshindwa kukata tamaa akisema kwamba bado ana uwezo wa kutinga hatua hiyo ya nne bora. “Sio jambo rahisi kwa klabu kubwa kushinda tatu ama nne mfululizo,” alisema kocha huyo.

    “Kwasababu hakuna ambaye ameshafanya hivyo, tuna nafasi ya kushinda na ndoto zetu ni kumaliza tukiwa miongoni mwa timu nne bora na kimahesabu inawezekana, tutajaribu kufanya hivyo.”

    Mbali na kujipa matumaini hayo, kocha uyo mwenye umri wa miaka 52 aliwapongeza mashabiki wa Chelsea ambao wameamua kuwa nae muda wote kwa kipindi hiki kigumu kwake.


    KOCHA aliye hatarini kupoteza kibarua chake, Jose Mourinho amesema kwamba bado anaamini timu yake ya Chelsea inaweza kuzinduka na kumaliza Ligi ikiwa nafasi ya nne bora. Hadi sasa, Chelsea wanashika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kucheza mechi 15, huku wakiwa wameshinda mechi moja kati ya sita za mwisho. Nafasi ya vijana hao wa Mourinho kufuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao ipo mashakani kutokana na kwamba wako nyuma kwa pointi 14 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi, Manchester United. Hata hivyo, pamoja na kuwa katika hali hiyo, kocha huyo raia wa Ureno ameshindwa kukata tamaa akisema kwamba bado ana uwezo wa kutinga hatua hiyo ya nne bora. “Sio jambo rahisi kwa klabu kubwa kushinda tatu ama nne mfululizo,” alisema kocha huyo. “Kwasababu hakuna ambaye ameshafanya hivyo, tuna nafasi ya kushinda na ndoto zetu ni kumaliza tukiwa miongoni mwa timu nne bora na kimahesabu inawezekana, tutajaribu kufanya hivyo.” Mbali na kujipa matumaini hayo, kocha uyo mwenye umri wa miaka 52 aliwapongeza mashabiki wa Chelsea ambao wameamua kuwa nae muda wote kwa kipindi hiki kigumu kwake.

    Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/licha-ya-kukalia-kuti-kavu-jose.html
    Copyright © saluti5
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LICHA YA KUKALIA KUTI KAVU, JOSE MOURINHO ANAAMINI CHELSEA ITATINGA TOP FOUR PREMIER LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top