728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, December 13, 2015

    MAZEMBE KUANZA KAZI LEO NA WAJAPAN

    TP Mazembe leo inaanza mashindano ya kusaka klabu bingwa dunia kwa kuwavaa mabingwa wa Japan, Sanfrecce Hiroshima, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Nagai jijini Osaka.

    Mechi hiyo ya robo fainali itakayotoa timu itakayopambana na River Plate katika nusu Fainali itaanza majira ya saa 7:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki


    Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu kutoka Japan, mshambuliaji wa kutumainiwa wa Mazembe, mtanzania Mbwana Samatta alikiri kuwa mechi ni ngumu kwavile wanapambana na mabingwa ambao pia wanacheza nyumbani kwao, ila wana uhakika wa kuibuka na ushindi na kuliwakilisha vema bara la Afrika.

    "Jamaa ni mabingwa wa hapa na si unajua wanacheza kwao bwana, ila tumejiandaa vizuri, mechi itakuwa ngumu ila Mungu atajalia tutawatoa tu."

    Mechi nyingine ya mapema itawakutanisha Club America na Guangzhou Evergrande mechi itakayopigwa majira ya saa 4:00 asubuhi hii katika uwanja huo huo wa Nagai.

      TBN_MUSSANKONINGO inawatakia kila la heri watanzania Samatta na Thomas Ulimwengu pamoja na timu yao ya Mazembe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAZEMBE KUANZA KAZI LEO NA WAJAPAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top