728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 7, 2015

    CHELSEA SIKIO LA KUFA, BAO LA UTATA LAIPA BOURNEMOUTH POINTI TATU STAMFORD BRIDGE ..(Picha)

    Ni wazi kuwa Chelsea inapoteza kabisa uwezo wa kutetea taji lake la Premier League baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bournemouth inayopapambana na janga la kushuka daraja. Ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani - Stamford Bridge, Chelsea ikazamishwa kwa bao la utata la dakika ya 82 kupitia kwa Glenn Murray ukiwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa tangu aingie uwanjani akitokea benchi. Bao la Glenn Murray limezua mjadala baada ya mchezaji huyo kufunga akiwa yeye na wavu huku akionekana wazi alikuwa ameotea. 
     
    Glenn Murray akiifungia Bournemouth dakika ya 82
    Glenn Murray akiifungia Bournemouth dakika ya 82

    Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/chelsea-sikio-la-kufa-bao-la-utata.html
    Copyright © saluti5

    Chelsea iko nyuma kwa pointi 14 kutoka kwa Manchester United inayoshikilia nafasi ya nne na ingawa timu kubwa bado hazijaonyesha njaa ya kusaka taji, lakini inahofiwa kuwa mabingwa hao watetezi wanaweza wakakosa hata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Kipa namba moja wa Chelsea Courtois aliyekuwa majeruhi kwa miezi kadhaa, amerejea uwanjani lakini uwepo wake haukumsaidia kocha Jose Mourinho kupokea kipigo cha nane msimu huu kwenye Premier League. Kwa mara nyingine tena mshambuliaji tegemeo wa Chelsea Diego Costa, alianzia benchi kabla ya kuingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Oscar. Chelsea: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Baba (Traore, 82), Fabregas (Remy 82), Matic, Willian, Oscar (Costa 46), Pedro, Hazard Bournemouth: Boruc, Smith, Francis, Cook, Daniels, Surman, Ritchie, Gosling, Arter, Stanislas, King (Murray 79)
     Tazama picha hapo chini.....







    Ni wazi kuwa Chelsea inapoteza kabisa uwezo wa kutetea taji lake la Premier League baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bournemouth inayopapambana na janga la kushuka daraja. Ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani - Stamford Bridge, Chelsea ikazamishwa kwa bao la utata la dakika ya 82 kupitia kwa Glenn Murray ukiwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa tangu aingie uwanjani akitokea benchi. Bao la Glenn Murray limezua mjadala baada ya mchezaji huyo kufunga akiwa yeye na wavu huku akionekana wazi alikuwa ameotea. Chelsea iko nyuma kwa pointi 14 kutoka kwa Manchester United inayoshikilia nafasi ya nne na ingawa timu kubwa bado hazijaonyesha njaa ya kusaka taji, lakini inahofiwa kuwa mabingwa hao watetezi wanaweza wakakosa hata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Kipa namba moja wa Chelsea Courtois aliyekuwa majeruhi kwa miezi kadhaa, amerejea uwanjani lakini uwepo wake haukumsaidia kocha Jose Mourinho kupokea kipigo cha nane msimu huu kwenye Premier League. Kwa mara nyingine tena mshambuliaji tegemeo wa Chelsea Diego Costa, alianzia benchi kabla ya kuingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Oscar. Chelsea: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Baba (Traore, 82), Fabregas (Remy 82), Matic, Willian, Oscar (Costa 46), Pedro, Hazard Bournemouth: Boruc, Smith, Francis, Cook, Daniels, Surman, Ritchie, Gosling, Arter, Stanislas, King (Murray 79)

    Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/chelsea-sikio-la-kufa-bao-la-utata.html
    Copyright © saluti5
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA SIKIO LA KUFA, BAO LA UTATA LAIPA BOURNEMOUTH POINTI TATU STAMFORD BRIDGE ..(Picha) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top