728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 7, 2015

    LICHA YA KUSHUTUMIWA KWA SOKA BOVU, VAN GAAL KUONGEZEWA MKATABA MANCHESTER UNITED

    Manchester United itafanya mazungumzo na kocha Louis van Gaal mwanzoni mwa mwaka mpya ili kuangalia uwezekano wa Mdachi huyo kusaini mkataba mpya Old Trafford. Licha ya kushutumiwa kwa soka bovu la Manchester United chini yake sambamba na tishio la kung'olewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku, wamiliki wa klabu hiyo pamoja na makamu mtendaji mkuu Ed Woodward, wanafurahia maendeleo yaliyoletwa na Van Gaal tangu achukue timu miezi 17 iliyopita. 

    Mkataba wa sasa wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, unatarajiwa kumalizika katikati ya mwaka 2017 na sasa United imeamua kufungua milango ya kurefusha mkataba huo. United inatarajiwa kuweka wazi mwelekeo wa hatma ya Van Gaal ndani ya miezi michache ijayo na tayari wako na mikakati mipya kwaajili ya msimu ujao. Mikakati hiyo itaipa Manchester United miezi 12 ya kutafuta mbadala wa Van Gaal iwapo ataamua kuondoka Old Trafford. Bodi ya Manchester United haitaki majanga ya kusaka kocha mpya kwa kukurupuka kama ilivyotokea baada Sir Alex Ferguson kustaafu ghafla mwaka 2013.

    Hapo awali Van Gaal alisisitiza kuwa hiki ni kibarua chake cha mwisho katika soka na anatarajiwa kuachana na kazi ya ukocha mara tu mkataba wake wa miaka mitatu United utakapomalizika ili kulinda ahadi aliyompa mkewe Truus.

    LICHA YA KUSHUTUMIWA KWA SOKA BOVU, VAN GAAL KUONGEZEWA MKATABA MANCHESTER UNITED

    Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/12/licha-ya-kushutumiwa-kwa-soka-bovu-van.html
    Copyright © saluti5
    Manchester United itafanya mazungumzo na kocha Louis van Gaal mwanzoni mwa mwaka mpya ili kuangalia uwezekano wa Mdachi huyo kusaini mkataba mpya Old Trafford. Licha ya kushutumiwa kwa soka bovu la Manchester United chini yake sambamba na tishio la kung'olewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku, wamiliki wa klabu hiyo pamoja na makamu mtendaji mkuu Ed Woodward, wanafurahia maendeleo yaliyoletwa na Van Gaal tangu achukue timu miezi 17 iliyopita. Mkataba wa sasa wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 64, unatarajiwa kumalizika katikati ya mwaka 2017 na sasa United imeamua kufungua milango ya kurefusha mkataba huo. United inatarajiwa kuweka wazi mwelekeo wa hatma ya Van Gaal ndani ya miezi michache ijayo na tayari wako na mikakati mipya kwaajili ya msimu ujao. Mikakati hiyo itaipa Manchester United miezi 12 ya kutafuta mbadala wa Van Gaal iwapo ataamua kuondoka Old Trafford. Bodi ya Manchester United haitaki majanga ya kusaka kocha mpya kwa kukurupuka kama ilivyotokea baada Sir Alex Ferguson kustaafu ghafla mwaka 2013. Hapo awali Van Gaal alisisitiza kuwa hiki ni kibarua chake cha mwisho katika soka na anatarajiwa kuachana na kazi ya ukocha mara tu mkataba wake wa miaka mitatu United utakapomalizika ili kulinda ahadi aliyompa mkewe Truus.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LICHA YA KUSHUTUMIWA KWA SOKA BOVU, VAN GAAL KUONGEZEWA MKATABA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top