728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 10, 2016

    Chadema kupinga marufuku ya mikutano mahakamani.




    Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema kuwa kitaenda mahakamani kupinga tangazo la hivi karibuni la polisi kwamba mikutano yote ya hadhara inyofanywa na upinzani imepigwa marufuku.

    Kulingana na gazeti la Citizen nchini Tanzania, uamuzi huo wa kwenda mahakamani ulitangazwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Saumu Mwalimu huko Mwanza.

    Inajiri baada ya mkutano wa siku mbili wa maafisa wakuu wa upinzani wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Freeman Mbowe.

    Gazeti hilo limesema kuwa maafisa wa Chadema na wabunge kadhaa wako katika mji huo wa Ziwa baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano katika eneo la Kahama siku mbili zilizopita.

    Maafisa wa polisi walisema kuwa mkutano huo ulioshirikisha chama cha ACT-wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa kigoma Zitto Kabwe utapigwa marufuku.

    Na siku ya Ijumaa Bw Malimu amesema kuwa watawasilisha kesi ya kutaka kubadilisha uamuzi huo wa polisi katika mahakama kuu Mwanza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Chadema kupinga marufuku ya mikutano mahakamani. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top