728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 6, 2016

    Rich Mavoko kaingia WCB, vipi kuhusu bifu la kulogana na Diamond.



    Msanii wa muziki Bongo, Rich Mavoko amesema aliamua kuungana na lebo ya WCB ya  msanii mwenzake Diamond Platnumz ili kuikuza tasnia ya muziki nchini.

    Akizungumzia tetesi za bifu na kulogana kati yake na Diamond, Rich ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa  ni watu wachache wenye kutaka kubomoa waliokuwa wakieneza habari hizi lakini hakukuwa na tatizo kati yao.

    “Naseeb tulikuwa na ushindani nae sana, tumehustle tumeangaika pamoja, hii ni kutaka kuachana na mambo yasiyo na faida na tufanye kazi kwa maslahi ya nchi” Alisema.

    Katika hatua nyingine, mmiliki huyo wa Hit ‘Imebaki Story’ alifunguka kwa kusema kuwa mkataba wake na WCB ni siri ila watu wategemee kazi nzuri kutoka kwao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Rich Mavoko kaingia WCB, vipi kuhusu bifu la kulogana na Diamond. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top