728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 7, 2016

    SHERIA YA MITANDAO IMEPUNGUZA PICHA ZISIZOFAA KWENYE MITANDAO.



    Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema kwamba  kuanza kutumika kwa sheria ya mitandao ya mwaka 2015 kumesaidia sana kupunguza uchochezi na picha zisizofaa kwenye mitandao.

    Ngonyani ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze juu ya manufaa yaliyopatikana tangu sheria hiyo kuanza kutumika.


    ”Sheria hii imesaidia sana mwanzoni kulikuwa na visa vilivoripotiwa polisi 459 ila baada ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo kesi zimepungua sana mfano kesi za uchochezi zilizoripotiwa ni nne, kesi ya moja ya kutoa taarifa zisizo sahihi, tukio moja tuu la video ya ngono jambo ambalo ni hatua kubwa ukilinganisha na hapo awali”-Amesema Ngonyani.

    Aidha Naibu Waziri amewataka wananchi watakapoona wamedhalilishwa kupitia mitandao ya kijamiii mara moja waripoti vituo vya polisi ili uchunguzi na kubaini wahusika uweze kufanyika mara moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHERIA YA MITANDAO IMEPUNGUZA PICHA ZISIZOFAA KWENYE MITANDAO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top