728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 27, 2015

    CHRISTIAN BELLA ADAI HATOI WIMBO MPYA ILI APATE TUZO.


    KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.
    KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ amefungukia ujio wake wa sasa wa Ngoma ya Amerudi aliyoizindua mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa hatoi wimbo mpya ili apate tuzo.

    Staa huyo anayebamba na Ngoma ya Nashindwa, aliwaambia mashabiki wa muziki wa Dansi waliokuwa wamefurika katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar katika uzinduzi wa wimbo wake huo wa audio na video kuwa anashangazwa na wasanii wanaokimbilia kutoa wimbo mpya ili wapate tuzo.
    “Kila siku nikilala nawaza mashabiki wangu nifanye nini muendelee kunipenda nisije kufulia. Nawaandalia ngoma kali na zinazodumu mwaka hadi mwaka.
    “Malaika Music ina miaka miwili sasa lakini ina wimbo mmoja tu uliofanya vizuri wa Nakuhitaji na wimbo huo una zaidi ya mwaka mpaka leo ukipigwa ni kama mpya. Leo (Ijumaa) tunazindua Amerudi na yenyewe itadumu miaka na miaka.“Wengi wanafikiria kutoa wimbo mpya ili wapate tuzo, sisi kwetu hatupo hivyo na hata mimi sipo kwa ajili hiyo,” alisema Bella.GPL(P.T)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHRISTIAN BELLA ADAI HATOI WIMBO MPYA ILI APATE TUZO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top