728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 29, 2015

    MAKUBWA YA EPL NEWCASTLE YALALA 1-O NYUMBANI DHIDI YA ARSENAL CHELSEA MAMBO SI SHWALI MAN CITY NAO WAPAA KILELENI WASHINDA 2-0 LEO.


    BAO la kujifunga la Fabricio Coloccini limeipa Arsenal ushindi wa ugenini Uwanja wa St James' Park dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Katika mchezo huo ambao Newcastle walimaliza pungufu baada ya Aleksandar Mitrovic kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 16, Fabricio Coloccini alijfunga baada ya kubabatizwa na mpira uliopigwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 52.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Arteta dk80, Ramsey, Sanchez na Walcott/Giroud dk70.
    Newcastle; Krul, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Haidara, Colback, Anita/Perez dk72, Thauvin/de Jong dk87, Wijnaldum, Sissoko/Cisse dk78 na Mitrovic.
    Tazama picha zaidi hapa chini.






     

    MANCHESTER CITY.
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Raheem Sterling amefunga bao kake la kwanza Manchetser City tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 49, timu hiyo ikishinda 2-0 dhidi ya Watford katika Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Etihad.
    Raheem Sterling aliyetokea Liverpool, alifunga bao lake hilo dakika ya 47 akimalizia krosi nzuri ya beki Mfaransa, Bacary Sagna.
    City ilipata bao la pili dakika 10 baadaye kupitia kwa Fernandinho aliyemalizia pasi maridadi ya kiungo wa Hispania, David Silva.
    Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Sagna, Mangala, Kompany, Kolarov, Fernandinho, Toure, Sterling/Iheancho dk90, Silva/Delph dk75, Navas/Nasri dk45 na Aguero.
    Watford; Gomes, Nyom, Prodl, Catchcart, Holebas, Behrami, Capoue/Watson dk76, Abdi/Anya dk63, Ighalo/Layun dk72, Jurado na Deeney.



     
    CHELSEA 
     
    BALAA gani hili. Kocha Mreno Jose Mourinho jioni ya leo hakuamini macho yake baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Crystal Palace nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge, London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao watetezi, Chelsea wazidiwe kwa pointi nane na vinara Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu.
    Bakary Sako alianza kuifungia Crystal Palace dakika ya 65 kabla ya Radamel Falcao kuisawazishia The Blues dakika ya 79 akimalizia krosi ya Pedro- lakini Joel Ward akawafungia wageni bao la ushindi dakika ya 81.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta/Kenedy, Fabregas, Matic/Loftus Cheek, Pedro, Hazard, Willian/Falcao na Diego Costa.
    Crystal Palace; McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Puncheon, Cabaye, McArthur, Zaha/Bolasie, Wickham na Sako.








     
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKUBWA YA EPL NEWCASTLE YALALA 1-O NYUMBANI DHIDI YA ARSENAL CHELSEA MAMBO SI SHWALI MAN CITY NAO WAPAA KILELENI WASHINDA 2-0 LEO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top