728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 27, 2015

    DADA WA KAZI WA PETER WA P SQUARE AFARIKI.


    “Esther alikuwa ni mfanyakazi bora kwenye familia yetu. Tulimpenda sana, tumejaribu kila dawa lakini Mungu ndiye aliyejua yote na hatuwezi kupingana naye” Hayo ni maneno yaliyoandikwa na Peter wa PsQuare kwenye mtandao wake wa kijamii wakati anatoa taarifa ya kifo cha mfanyakazi wake wa ndani.
    Kifo cha mfanyakazi huyo kimetokea leo asubuhi ambapo kwa muda wa miaka 5 alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa.
    Peter na Mke wake Lola Omotayo wameishi na Esther kwa muda wa miaka 7 ambaye ndiye alikuwa akiwasaidia kufanya kazi zao za ndani hususani kulea mtoto wao.
    Kutokana na kushuhudia mateso aliyokuwa nayo Esther Peter ametoa ushauri kwa wakina dada kwenda kupima afya zao ili kufahamu mapema kama wanavinasaba vya ugonjwa wa kansa au la, na kama mtu akigundulika ni bora aanze tiba mapema
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DADA WA KAZI WA PETER WA P SQUARE AFARIKI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top