728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 29, 2015

    NDANDA FC WATOA SARE NA AZAM FC (NDANDA DAY)



    Ndanda FC leo wamekamilisha siku yao maalum kwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Azam Fc, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara.
    Katika mchezo huo wa kirafiki Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Kelvin Friday katika dakika ya 12 na kuipelekea Azam FC kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
    Katika dakika ya 70 NDanda FC walipata penati kufuatia David Mwantika kumfanyia madhambi Atupile Green na penati hiyo kupaishwa na Kigi Makasi, huku Mwantika akizawadiwa kadi nyekundu.
    Ndanda FC walipata goli lao la kusawazisha katika dakika ya 80 kupitia kwa Omar Mponda na kupeleka mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NDANDA FC WATOA SARE NA AZAM FC (NDANDA DAY) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top