728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 25, 2015

    STARS YAANZA KUJIFUA VEMA UTURUKI.

    Wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Abdi Banda, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub.
    Wachezaji wa timu ya taifa TAIFA STARS.

    Viungo ni Frank Domayo, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla na washambuliaji ni Saimon Msuva, Deus Kaseke, John Bocco, Rashid Mandawa na Farid Musa na Ibrahim Hajibu. Mlinda mlango Aishi Manula hakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya jumamosi kati ya timu yake Azam FC dhidi ya Yanga SC.

                                               
    Ni Mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Yanga SC. Ni miongoni mwa makipa bora kabisa kwa sasa nchini Tanzania.
    Bathez kama anavyofahamika kwa washabiki na wapenzi wa mpira wa miguu ukanda wa Afrika Mashariki, amekua akiitumikia timu ya Taifa kwa vipindi mbali mbali tangu mwaka 2008.
    Uwezo wake wa kuwapanga mabeki na kuongea nao wakati wa mchezo, kuokoa michomo ya hatari kutoka kwa washambuliaji, imeendelea kuwa sifa kubwa kwa mlinda mlango huyo ambaye pia amewahi kuzichezea timu za Simba SC na Ashanti United za jijini Dar es salaam.
    Kipa huyo ni kipa wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013, 2014/2015 na washindi wa Ngao ya Jamii 2015/2016. Licha ya kutwaa ubingwa huo wa VPL akiwa na Yanga pia aliwahi kutwaa ubingwa huo akiwa na klabu ya Simba SC. Aidha kipa huyo pia ni mshindi wa kombe la Kagame mwaka 2012.
      
    Mustafa Barthez.
    Barthez ana uzoefu mkubwa katika mashindano ya kimataifa, kwani ameshafanikiwa kucheza michezo mingi yenye upinzani wa hali ya juu katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa.
    Kuelekea mchezo dhidi ya Nigeria, mlinda mlango huyo yupo vizuri na endapo mwalimu atampa nafasi atafanya vizuri katika kuperusha bendera ya Taifa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STARS YAANZA KUJIFUA VEMA UTURUKI. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top