728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 23, 2015

    ENDAPO ZIKIFUATWA SHERIA HIZI SAHIHI AJALI ZA BARABARANI ZITAPUNGUA TU BEST WANGU.




    Wananchi katika manispaa ya TABORA wametakiwa kufuata matumizi sahihi ya barabara ikiwa ni pamoja na sheria za barabarani ili kuepusha ajali za barabarani.


    Wito huo umetolewa na Afisa Mfawidhi wa  Mmlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini -SUMATRA Bwana JOSEPH MICHAEL wakati akizungumza na  na CG FM ofisini kwake kuhusu uelewa wa wananchi juu ya elimu ya usalama barabarani.


    Amewataka wananchi kufuata matumizi sahihi ya barabara na kuacha kutumia barabara kwa mazoea.

    Bwana MICHAEL pia amewahimiza wanawake wenye mazoea ya kupanda baiskeli huku wakiwa na watoto mgongoni kuacha tabia hiyo na kusema kuwa ni hatari kwa usalama wao hasa wanapokua barabarani.


    MARIA PETER,YAHAYA SAIDI,na SAMWELI ni baadhi ya  wakazi wa manispaa ya TABORA wamesema ukosefu  wa elimu na ukosefu  wa miundo  mbinu ya alama za barabara ndiyo chanzo cha watu  kutofuata matumizi sahihi ya barabara na hivyo kusababisha ajali nyingi za barabarani. 


    Uelewa mdogo wa matumizisahihi ya barabarani kwa wananchi umekua ukisababisha ajali za mara kwa mara katika maeneo mengi nchini.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ENDAPO ZIKIFUATWA SHERIA HIZI SAHIHI AJALI ZA BARABARANI ZITAPUNGUA TU BEST WANGU. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top