Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
amesema kuwa ataweka sahihi ya makubaliano ya amani siku ya jumatano
baada ya kukataa kufanya hivyo wiki iliopita.
Msemaji wa Salva
Kiir amesema kuwa rais huyo ataweka sahihi yake ya makubaliano hayo
katika mji mkuu wa Juba mbele ya viongozi wa eneo hili.Salva Kiir anakabiliwa na vikwazo pamoja na kikwazo cha umoja wa mataifa cha kutonunua silaha baada ya kukataa kuidhinisha makubaliano hayo.
Mpinzani wake ambaye ndio kiongozi wa waasi Riek Machar tayari ameweka sahihi mkataba huo ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miezi 20.
BBC.
0 comments:
Post a Comment