BAO
la kujifunga la Fabricio Coloccini limeipa Arsenal ushindi wa ugenini
Uwanja wa St James' Park dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi
Kuu ya England.
Katika
mchezo huo ambao Newcastle walimaliza pungufu baada ya Aleksandar
Mitrovic kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 16, Fabricio Coloccini
alijfunga baada ya kubabatizwa na mpira uliopigwa na Alex
Oxlade-Chamberlain dakika ya 52.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal,
Coquelin, Cazorla, Oxlade-Chamberlain/Arteta dk80, Ramsey, Sanchez na
Walcott/Giroud dk70.
Newcastle;
Krul, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Haidara, Colback, Anita/Perez dk72,
Thauvin/de Jong dk87, Wijnaldum, Sissoko/Cisse dk78 na Mitrovic.
Tazama picha zaidi hapa chini.
MANCHESTER CITY.
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa England, Raheem Sterling amefunga bao kake la kwanza
Manchetser City tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 49, timu hiyo
ikishinda 2-0 dhidi ya Watford katika Ligi Kuu ya England jioni ya leo
Uwanja wa Etihad.
Raheem Sterling aliyetokea Liverpool, alifunga bao lake hilo dakika ya 47 akimalizia krosi nzuri ya beki Mfaransa, Bacary Sagna.
City
ilipata bao la pili dakika 10 baadaye kupitia kwa Fernandinho
aliyemalizia pasi maridadi ya kiungo wa Hispania, David Silva.
Kikosi
cha Manchester City kilikuwa; Hart, Sagna, Mangala, Kompany, Kolarov,
Fernandinho, Toure, Sterling/Iheancho dk90, Silva/Delph dk75,
Navas/Nasri dk45 na Aguero.
Watford;
Gomes, Nyom, Prodl, Catchcart, Holebas, Behrami, Capoue/Watson dk76,
Abdi/Anya dk63, Ighalo/Layun dk72, Jurado na Deeney.
CHELSEA
BALAA
gani hili. Kocha Mreno Jose Mourinho jioni ya leo hakuamini macho yake
baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Crystal Palace nyumbani Uwanja wa
Stamford Bridge, London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Matokeo
hayo yanawafanya mabingwa hao watetezi, Chelsea wazidiwe kwa pointi
nane na vinara Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu.
Bakary
Sako alianza kuifungia Crystal Palace dakika ya 65 kabla ya Radamel
Falcao kuisawazishia The Blues dakika ya 79 akimalizia krosi ya Pedro-
lakini Joel Ward akawafungia wageni bao la ushindi dakika ya 81.
Kikosi
cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Zouma, Cahill,
Azpilicueta/Kenedy, Fabregas, Matic/Loftus Cheek, Pedro, Hazard,
Willian/Falcao na Diego Costa.
Crystal Palace; McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare, Puncheon, Cabaye, McArthur, Zaha/Bolasie, Wickham na Sako.
0 comments:
Post a Comment