Wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki ni magolikipa Ally Mustafa,
Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed
Hussein, Hassan Isihaka, Abdi Banda, Kelvin Yondani na nahodha Nadir
Haroub.
Wachezaji wa timu ya taifa TAIFA STARS. |
Viungo ni Frank Domayo, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said
Ndemla na washambuliaji ni Saimon Msuva, Deus Kaseke, John Bocco,
Rashid Mandawa na Farid Musa na Ibrahim Hajibu. Mlinda mlango Aishi
Manula hakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi baada ya
kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii siku ya jumamosi kati ya timu yake
Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Ni Mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Yanga SC. Ni miongoni mwa makipa bora kabisa kwa sasa nchini Tanzania.
Bathez kama anavyofahamika kwa washabiki na wapenzi wa mpira wa miguu
ukanda wa Afrika Mashariki, amekua akiitumikia timu ya Taifa kwa
vipindi mbali mbali tangu mwaka 2008.
Uwezo wake wa kuwapanga mabeki na kuongea nao wakati wa mchezo,
kuokoa michomo ya hatari kutoka kwa washambuliaji, imeendelea kuwa sifa
kubwa kwa mlinda mlango huyo ambaye pia amewahi kuzichezea timu za Simba
SC na Ashanti United za jijini Dar es salaam.
Kipa huyo ni kipa wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2012/2013, 2014/2015 na washindi wa Ngao ya Jamii 2015/2016. Licha ya
kutwaa ubingwa huo wa VPL akiwa na Yanga pia aliwahi kutwaa ubingwa huo
akiwa na klabu ya Simba SC. Aidha kipa huyo pia ni mshindi wa kombe la
Kagame mwaka 2012.
Mustafa Barthez. |
Kuelekea mchezo dhidi ya Nigeria, mlinda mlango huyo yupo vizuri na
endapo mwalimu atampa nafasi atafanya vizuri katika kuperusha bendera ya
Taifa
0 comments:
Post a Comment