Teknolojia imefanikiwa kuleta mambo mapya karibu kwenye kila kitu, tumezoea kuona magari yanatumia petrol na diesel, yakagunduliwa magari yanayotumia gesi, sasahivi yapo mpaka yanayotumia umeme !!
Huenda kama una safari ndefu na gari lako linatumia umeme ukapata stress nyingine, kwa mfano gari likiisha chaji katikati ya safari inakuwaje??
Teknolojia imefika pazuri, tunatambulishwa kwenye hizi barabara mpya, za kisasa kabisa ambazo kama unaendesha gari inayotumia umeme basi ukipita kwenye upande huo wa barabara gari inaendelea kuingiza chaji huku safari yako ikiendelea kwa amani zote kabisa !!
Kwenye Jiji la Gumi, Korea Kusini kuna mabasi ya abiria ambayo yanatumia mfumo wa umeme, wao wameweka switch kwa ajili ya magari yanayotembea umbali wa kama Kilometa 25 wanakutana na cable za umeme kwa ajili ya kuchajia gari, hizo cable zimepitishwa chinichini na umeme wake.
Uingereza wako kwenye mipango kuweka hizo cable kila baada ya umbali wa kama Kilometa 32 hivi, ila mpango mkubwa zaidi walionao ni huu wa kuanza kutumia hizo barabara ambapo hakuna gari nyingine itaruhusiwa kupita upande huo wa barabara.
Utaalam mwingi sana uko hapo aisee, unaambiwa gari haitasimama ili kuingiza chaji wala haitachomekwa cable za umeme.. chaji itaendelea kujaa kwenye gari kama inavyochaji simu kwa mfumo wa Wireless !!
Kuna sehemu tayari ndani ya Uingereza wamekamilisha ujenzi wa barabara hizo na majaribio yatafanyika muda si mrefu ndani ya mwaka huuhuu 2015… Unatamani hii ifike na Bongo mtu wangu?
0 comments:
Post a Comment