Wasichana wapatao 38 wamekufa katika
ajali ya gari nchini Swaziland wakati walipokuwa wakisafiri kwenda
kwenye sherehe ya kitamaduni.
Shirika la kutetea haki za binadamu
nchini Swaziland, Solidarity Network limesema wasichana hao waliokufa
walikuwa wamejeruhiwa vibaya wakati gari lao lilipogongana na gari
jingine siku ya Ijumaa.
Walikuwa njia kwenda katika jumba la mfalme wa nchi hiyo katika ngoma maarufu ya kitamaduni.
Kila mwaka kiasi cha wasichana wapatao elfu arobani hushiriki kwenye sherehe hizo za kitamaduni za siku nane.
Hupita
mbele ya mfalme wakiwa nusu uchi. Mashirika ya kutetea haki za binadamu
wamekuwa wakipinga sherehe hizo kwa kusema zimepitwa na wakati na ni za
king'ono.
BBC
0 comments:
Post a Comment