LEO zimetimia siku 500
tangu wanafunzi zaidi ya 200 wa kike walipotekwa nyara na kundi la
kigaidi la Boko Haram kutoka mji cha Chibok kaskazini-mashariki mwa
Nigeria, huku matumaini ya kupatikana kwa wanafunzi hao yakizidi
kufifia.
Kumbukumbu hiyo inafanyika wakati hali ya usalama ikizidi kuwa mbaya
katika eneo hilo, ambako Boko Haram wamezidisha mashambulizi tangu
kuingia madarakani kwa rais Muhammadu Buhari, ambapo wameuwa zaidi ya
watu 1,000 katika miezi mitatu.
Wapiganaji hao walivamia shule ya serikali mjini Chibok katika jimbo
la Borno jioni ya Alhamis 14 mwaka jana, na kuwateka wanafunzi 276
waliokuwa wanajiandaa na mitihani yao ya mwisho wa mwaka.
0 comments:
Post a Comment