RUDISHA. |
David Rudisha
alikabili maswali mengi kuhusu uwezo wake wa kuimarika katika mbio za
mita 800 baada ya kushinda dhahabu katika mashindano ya riadha ya
Beijing.
Bingwa huyo wa mbio za Olimpiki na bingwa wa rekodi ya
dunia katika mbio hizo ambaye pia alishinda taji la ulimwengu mwaka
2011,aliongoza kutoka mbele na kuweza kuweka mda wa dakika 1sekunde
45.84 mbele ya mwanariadha wa Poland Adam Kszczot.
Amel Tuka wa Bosinia Haerzegovina ambaye anashikilia mda bora mwaka huu alichukua medali ya shaba.
Hatahivyo
mbio hizo zilikosa msisimuko wake baada ya mwanariadha wa Botswana
Nijel Amos na mwenzake wa Ethiopia Mohammed Aman kushindwa kufuzu katika
fainali.
DIBABA |
Wakati huohuo Mkenya Nicholas Bett alinyakua medali
ya dhahabu baada ya kuweka mda bora wa sekunde 47.79 katika mashindano
ya mbio za mita 400 kuruka viunzi.
Raia wa Urusi Denis Kudryavtsev alichukua medali ya fedha huku Jeffery Gibson wa Bahamas akimaliza wa tatu.
Ilikuwa medali ya kwanza ya Kenya katika mbio fupi katika mashindano ya dunia.
Katika upande wa wanawake mwanariadha wa Ethiopia Genzebe Dibaba alichukua dhahabu katika mbio za mita 1500.
BETT |
Muingereza Laura Muir alimaliza wa tano katika mbio
na Paula Radcliff na kuongezea kuwa raia huyo wa Uskochi anaweza
kuondoka Beijing akiwa na furaha.
Faith Chepngetich Kipyegon alichukua nafasi ya pili huku Sifan Hassan wa Uholanzi akimaliza wa tatu.
0 comments:
Post a Comment