728x90 AdSpace

Tuesday, August 25, 2015

BAADA YA KUICHACHAFYA SIMBA SASA KUPIMANA NA AZAM FC.

kikosi cha azam fc

Azam FC na timu mpya kwenye ligi kuu ya Mwadui FC ya 
Shinyanga kesho usiku zitakwaana kwenye uwanja wa Azam Complex katika mechi ya kirafiki kujiandaa na ligi kuu.
Mashabiki wa soka nchini watapata nafasi kuiona mechi hii live kupitia moja ya chaneli za Azam TV.
Azam FC ambayo imepoteza wachezaji wake wengi walio na timu ya taifa itatumia mechi ya kesho kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye mechi nyingi zilizopita huku kwa Mwadui FC timu iliyotoka sare ya 0-0 na Simba jana itatumia mechi hiyo kuendelea kuwaweka pamoja wachezaji wake ambao wengi ni wapya.
Wakati huo huo, wacheaji Ismail Adam Gambo na Omary Wyne wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji ya huko kwa mkopo.
Hii ni nafasi muhimu kwa wachezaji hawa wenye vipaji toka Academy ya Azam FC kupata fursa ya kucheza ligi kuu na kupata changamoto mpya baada ya kutumia takribani miaka mitatu kwenye academy wakijifunza soka.
Wachezaji hawa pia ni wanandinga wa timu za taifa za vijana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: BAADA YA KUICHACHAFYA SIMBA SASA KUPIMANA NA AZAM FC. Rating: 5 Reviewed By: Unknown