Bado michuano maalum ya Copa America 2016 ambayo inatumika kama kusherehekea miaka 100 ya mashindano hayo inaendelea, kama ulikuwa hujui alfajiri ya June 11 Argentina ilicheza dhidi ya Panama katika mchezo wake wa pili wa Kundi D.
Katika mchezo huo Argentina walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-0, ushindi ambao ulipatikana baada ya nahodha wao Lionel Messi kuingia katika mchezo huo dakika 29 za mwisho, kuingia kwa Messi kulikuwa kuna madhara makubwa kwa Panama, kwani ilionekana mabeki wao kushindwa kumdhibiti staa huyo.
Messi ndio mchezaji aliyesababisha kuidhoofisha zaidi Panama, kwani uwepo wake uwanjani ulifanya apachike magoli matatu yaani hat-trick dakika ya 68, 78 na 87, baada ya Nicolas Otamendi kupachika goli la kwanza dakika ya 7 na Sergio Aguero kuhitimisha furaha ya waargentina baada ya kupachika goli la mwisho dakika ya 90.
Hata hivyo Panama walilazimika kumalizia dakika 59 za mchezo kwa kucheza wakiwa na wachezaji 10 uwanjani, hiyo inatokana na mchezaji wao mmoja Anibal Godoy
kuoneshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 31 na kutolewa nje ya uwanja
kutokana na kucheza faulo akiwa tayari alionywa kwa kadi ya kwanza ya
njano.
Tazama video ya magoli yote Hapa chini.
0 comments:
Post a Comment