Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
amesema kwamba kuanza kutumika kwa sheria ya mitandao ya mwaka
2015 kumesaidia sana kupunguza uchochezi na picha zisizofaa kwenye
mitandao.
Ngonyani ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Chalinze juu ya manufaa yaliyopatikana tangu sheria hiyo kuanza kutumika.
”Sheria hii imesaidia sana mwanzoni kulikuwa na visa vilivoripotiwa
polisi 459 ila baada ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo kesi zimepungua
sana mfano kesi za uchochezi zilizoripotiwa ni nne, kesi ya moja ya
kutoa taarifa zisizo sahihi, tukio moja tuu la video ya ngono jambo
ambalo ni hatua kubwa ukilinganisha na hapo awali”-Amesema Ngonyani.
Aidha Naibu Waziri amewataka wananchi watakapoona wamedhalilishwa kupitia mitandao ya kijamiii mara moja waripoti vituo vya polisi ili uchunguzi na kubaini wahusika uweze kufanyika mara moja.
0 comments:
Post a Comment