Ligi
kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16 imekwisha kwa kishindo huku Young
Africans wakiibuka mabingwa kwa mara nyingine na kuna baadhi ya wachezaji
walionyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka kupitia klabu zao.
Kutokana
na umahiri waliouonyesha kwa kipindi cha msimu mzima, mtandao huu unakuletea
kikosi cha wachezaji 11 bora.
1.
Aishi
Manula
Manula
anastaili kuwa kipa bora wa ligi ya msimu wa 2015/16, kutokana na mchango
mkubwa alioutoa kwa timu yake katika mashindano yote aliyoichezea timu hiyo
msimu huu.
Manula
ndiye kipa aliyeidakia Azam FC mechi nyingi za ligi kuliko msaidizi wake
Mwadini Ali, lakini pia kipa huyo aliipa ubingwa wa Kombe la Kagame timu hiyo
bila kufungwa hata bao moja na pia alifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari nyingi
kwenye lango la Azam ilipocheza na Esperance ya Tunisia kwenye michauano ya
Kombe la Shirikisho Afrika.
2.
Juma
Abduli
Beki
wa Young Africans anayetajwa kuwa mchezaji bora msimu huu kutokana na mchango
wake kwenye kikosi cha Young Africans na hata timu ya taifa, mabao mengi
yaliyofungwa na Amissi Tambwe na Donald Ngoma yametokana na krosi za Juma
ambazo mara zote zimekuwa na matunda kutokana na utaalamu aliokuwa nao.
3.
Mohamed
Hussein ‘Tshabalala’
Mchezaji
bora wa mwezi Aprili wa klabu ya Simba ambaye licha ya kuwa na umbo dogo lakini
amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, beki huyo wa kushoto
ameonyesha uwezo mkubwa wa kuwadhibiti washambuliaji wakorofi lakini pia
ameonyesha uwezo wa kupanda mbele kupiga krosi nyingi ambazo zilisababisha
hatari kwenye lango la timu pinzani.
4.
Andrew
Vicent ‘Dante’
Mlinzi
makini kwenye safu ya ulinzi ya timu ya Mtibwa Sugar ambaye amefanya vizuri
msimu huu na kuisaidia timu yake kufanya vizuri kwenye mashindano yote
iliyoshiriki ingawa haikuweza kubeba taji lolote kati ya hayo.
Uwezo
wa Dante, ulionekana zaid pale alipofanikiwa kumdhibiti mshambuliaji wa Young
Africans Donald Ngoma asipeleke madhara kwa kipa wake Said Mohamed katika
mchezo wa marudiano wa ligi, ingawa mchezo huo Young Africans walishinda kwa
bao 1-0.
5.
Pascal
Wawa
Beki
mahiri mwenye uwezo mkubwa anayeichezea klabu ya Azam FC, ameingia kwenye
kikosi hiki kutokana na uwezo aliokuwa nao na mchango wake kwa Azam haina
ubishi uwepo wa Wawa kuna ongeza hata uimara wa kipa Aishi Manula.
Mlinzi
huyu wa kati kutoka Ivory Coast, amekuwa akicheza kwa kujitoa na kusaidia sana
mafanikio ya timu hiyo kwa msimu mmoja na nusu ambao tayari ameichezea timu
hiyo na ukitaka kuona kama anamchango mkubwa kwenye timu hiyo angalia pale
alipoumia na kukosa mechi za mwishoni mwa msimu huu timu hiyo haikuwa na
mwenendo mzuri kiasi cha kupoteza hata mbio za ubingwa na kufungwa mabao 3-1 na
Young Africans kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la FA.
6.
Jean
Baptiste Mugiraneza
Huyu
ni kiungo Mnyarwanda anayeichezea klabu ya Azam amekuwa akifanya kazi kubwa
kuipigania timu yake hiyi tangu alipojiunga nayo mwanzoni mwa msimu akitokea
APR.
Akiwa
katika msimu wake wa kwanza tayari ameonyesha kama yeye ni hodari kwa
kuweza kuimudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji na kuwaweka benchi wachezaji
Frank Domayo na Michael Bolou ambao walikuwa wakijinafasi hapa awali kabla ya
ujio wake.
7.
Farid
Mussa
Winga
hatari kabisa ambaye kiwango alichokionyesha msimu huu hakina mpinzani na
kinamfanya kuingia kwenye kikosi bora cha msimu huu pasipo kupigwa kutokana na
mchango alioutoa kwa timu yake ya Azam lakini pia timu ya taifa.
Mussa
analazimika kumshukuru kocha Stewart Hall wa Azam ambaye alichangia kupandisha
kiwango chake na hivi karibuni mchezaji huyo huenda akajiunga na timu ya
Tenerife Deportivo inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania baada ya
kufuzu majaribio aliyofanya kwa wiki tatu .
8.
Thabani
Kamusoko
Tangu
atue kwenye kikosi cha Young Africans msimu huu bado hajaonekana mchezaji
mwingine wa nafasi ya kiungo mchezeshaji atakaye weza kumuondoa kwenye nafasi
hiyo Mzimbabwe huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kutoa pasi na
kuichezesha timu lakini hata kufunga.
Kiwango
kilichoonyeshwa na Kamusoko kinamfanya kumuweka pembeni Haruna Niyonzima
na kuchukua nafasi hiyo kutokana na umahiri wake wa ukabaji kuisaidia safu ya
ulinzi kupunguza presha ya mashambulizi.
9.
Amissi
Tambwe
Idadi
ya mabao 21 aliyoifungia Young Africans msimu huu ni wazi anastaili kuwa kwenye
kikos cha wachezaji 11 bora waliofanya vizuri msimu huu uliomalizika siku za
karibuni.
Tambwe
amekuwa akipondwa kuwa ni mchezaji wa kawaida lakini amekuwa na madhara makubwa
anapokuwa kwenye lango la timu pinzani uwezo wake wa kufunga kwa kutumia kichwa
na miguu umemfanya kuibuka mfungaji bora kwa mara ya pili akiwa na timu za
Simba na Young Africans.
10.
Donald
Ngoma
Hapana
shaka kiwango kilichoonyeshwa na Donald Ngoma kimekata kiu ya mashabiki wa timu
hiyo kuiona timu yao ikiwa na mtu ambaye inaweza kujivunia kama wapinzani wao
Simba walivyokuwa wakijitambia walipokuwa na Emmanuel Okwi.
Sifa
kubwa aliyoiweka Ngoma msimu huu nu kuzifunga timu zote kubwa kubwa Azam,
Simba, Mtibwa Al Ahly na APR, huku akionyesha uwezo mkubwa wa kupambana na
kumaliza nafasi ya tatu kwa ufungaji bora sifa hizo zinamfanya Mzimbabwe huyo
kuingia kwenye kikosi hicho na kutokana na uwezo aliokuwa nao.
11.
Shizza
Kichuya
Winga
hatari wa Mtibwa Sugar amekuwa na msimu mzuri kiasi cha kumshawishi kocha wa
timu ya taifa ya bTanzania Boniface Mkwassa kumjumuisha kwenye kikosi chake
kitakachovaana na Misri Jumamosi hii.
Kichuya
ameingia kwenye kikosi hiki bora msimu huu kutokana na cnhango alioutoa kwa
timu yake ya Mtibwa kwenye mashindano yote waliyoshiriki msimu huu ikiwemo
michuano ya Kombe la mapinduzi ambapo walifungwa na URA ya Uganda kwenye mchezo
wa fainali.
0 comments:
Post a Comment