Kiongozi wa upinzani nchini Uganda
Dk.Kizza Besigye aliyekuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu
shtaka la uhaini hajafikishwa mahakamani.
Upande wa mashtaka umeomba ruhusa mahakama hiyo ihamishwe karibu na
gereza alikozuiliwa bw Besigye kwa ajili ya tishio la amani mjini.
Hata hivyo viongozi wengine wa upinzani wamejaa mahakamani ambapo wanafanya mgomo baridi.
Hakimu aliyekuwa anatarajiwa kusikiza kesi hiyo aliagiza kuahirishwa
kwa kusikizwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi huu wa sita.
Bw Besigye ndiye aliyekuwa mshindani wa karibu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa February 2016.
Kiongozi huyo wa upinzani anadai kuwa alishinda katika uchaguzi huo, ambao ulikosolewa na wangalizi wa kimataifa.
Hatua yake ya kujiapisha kuwa rais ndiyo iliyomkasirisha rais
Museveni ambaye ndiye ameanza hatamu yake ya tano uongozini na
kusababishwa kukamatwa kwake kwa kukiuka katiba kwa kosa la uhaini.
Besigye amekuwa akishikiliwa na polisi kwa muda wa siku kumi na mbili
baada ya mahakama huko Moroto kuagiza awekwe rumande hadi Juni mosi.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.
0 comments:
Post a Comment