Timu ya taifa ya Misri, Pharaos, inatarajiwa kuwasili nchini leo
Jumatano kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya
Afrika (Afcon 2017) dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Mchezo huo wa Kundi G unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar, Misri ndiyo wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi saba wakifuatiwa
na Nigeria wenye pointi mbili Tanzania ni ya tatu ikiwa na pointi moja,
hivyo inahitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kufuzu.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas, alisema
kuwa kwa asilimia kubwa maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na
wamejipanga vizuri kuwapokea wageni wao hao.
“Timu ya Misri watafika kesho (leo) lakini bado hawajatuambia muda
gani watakuja, kila kitu kipo vizuri, huu ni mchezo muhimu kwa Srars
kwani kwa vyovyote vile inatakiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo,”
alisema Lucas.
Mbali na hilo Lucas pia alisema: “Timu yetu ya taifa ya wanawake,
Twiga Stars, inatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kucheza mechi ya
kirafiki, mchezo ambao unatarajiwa kupigwaJune 17 mwaka huu, watautumia
mchezo huo kwa maandalizi ya mechi zao za kuwania kupata nafasi ya
kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake hapo mwakani.”
0 comments:
Post a Comment